#bravotv_tz

552 posts

Loading...
JESHI LA POLISI LAKIRI KUMBAMBIKIA KESI MFANYABIASHARA TABORA - Jeshi la Polisi nchini, limekiri kuwa taarifa za awali walizopata kutoka Mkoani Tabora zimeonesha kwamba askari wake walimbambikia kesi mfanyabiashara, Mussa Sadiki - Mfanyabiashara huyo ni yule ambaye juzi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga, alimzungumzia kuwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi walimbambikia kesi ya mauaji huko Tabora - Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, alisema awali walipokea barua ya malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara huyo na Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilimtuma ofisa wake mwenye cheo cha juu kwenda Tabora kufanya uchunguzi na kwamba hadi sasa anaendelea kuukamilisha ili hatua zichukuliwe dhidi ya waliohusika - Kwa mujibu wa malalamiko yaliyoandikwa kwenye gazeti, mtuhumiwa baada ya kukamatwa aliwekwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Tabora kwa kumbambikizia kesi ya kuvunja na kuiba na alikaa kituoni kwa wiki moja na alipopelekwa Mahakamani, alisomewa shtaka la mauaji #bravotv_tz
Raia wa Algeria wakiandamana katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo Algiers wakihofia Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika (82) ana mpango wa kuendelea kusalia madarakani baada ya kuliongoza Taifa hilo toka mwaka 1999.#bravotv_tz (📹 AFP TV)
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imesaini Mkataba wa Ushirikiano na Hospitali ya Jimbo la Shandong na hospitali bingwa ya moyo ya FUWAI.Taasisi hizo zimekubaliana kubadilishana uzoefu katika tiba ya moyo; na wataalam mabingwa kutoka #China watakwenda kufanya upasuaji . #bravotv_tz
Baada Ya Kisanduku cha kutunza kumbukumbu,Sauti Na Data za ndege ‘Black Box’ cha ndege ya #EthiopianAirlines Boeing 737 Max 8 kupatikana . . Kifaa hicho Muhimu Kimesafirishwa Mjini #Paris Ufaransa Tayari Kwa Uchunguzi Kugundua Nini Haswa Chanzo Cha Ajali Hio,Ufaransa Ni Watengenezaji Wa Ndege Aina Za Airbus Hivyo Watasema Ukweli , Wakati Marekani Wanatengeneza Ndege Aina Ya Boeing . #bravotv_tz
BAADA YA KUTOKA GEREZANI MBOWE AKUTANA NA JINGINE KILA KUKICHA AFADHARI YA JANA Wamiliki 34 wa viwanja katika eneo la maendelezo ya viwanda la Weruweru katika Wilaya ya Hai, mkoani #Kilimanjaro akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wako ‘njia panda kufuatia kudaiwa kodi ya pango la ardhi. Mbowe na walimiki wengine wako njia panda, baada ya Mkuu wa Wilaya ya #Hai , Lengai Ole Sabaya kutangaza hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kuwa ni pamoja na ilani ya ubatilisho wa umiliki wao kutumwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. Akitangaza orodha hiyo, wakati wa mkutano wa siku mbili wa kusikiliza kero, malalamiko na migogoro ya ardhi, Sabaya amesema watu hao wamo katika orodha ndefu ya wamiliki ambao viwanja vyao vimeombewa kibali cha kufutwa. Idadi hiyo ya watu 34, inafanya jumla ya kiasi cha fedha kinachodaiwa kutokana na pango la ardhi kufikia Shilingi 1, 828, 166, 096. Mbali na Mbowe wamo pia Mkuu wa mkoa wa zamani wa Kilimanjaro, Cynthia Hilda Ngoye, Kiwanda cha Kutengeneza Vipuri cha Kilimanjaro Mashine Tools Manufacturing Company Ltd kilichopo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na wafanyabiashara maarufu wa mji wa Moshi wanaomiliki shule binafsi na makampuni ya utalii. #bravotv_tz
Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amesema serikali itaendelea kuvichukulia hatua vyuo vikuu vitakavyoshindwa kukidhi masharti ya utoaji wa elimu ya juu ili kuhakikisha Tanzania inazalisha wasomi wenye ubora wa uhakika #bravotv_tz
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat Abdulrazak Ofisini kwake Jijini #Dodoma , #bravotv_tz
Cleopa Msuya ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania ambaye alihudumu kama Waziri Mkuu katika Serikali mbili tofauti ikiwemo ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere kuanzia 1980 - 1983 na 1994-1995 chini ya Rais Mwinyi. #bravotv_tz
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi anatarajia kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Windhoek Namibia kuanzia Machi 15 hadi 17. #bravotv_tz
BRAZIL: WATU 8 WAUAWA KWA RISASI KWENYE SHULE MOJA YA MSINGI - Vijana wawili wakiume wa miaka 17 na 25 walivamia shule ya msingi Raul Brazil iliyopo Sao Paulo hapo jana na kushambilia watu kwa risasi na kisha kujiua wenyewe - Waliouawa ni pamoja na watoto watano, Wafanyakazi wawili wa shule hiyo na mmiliki wa sehemu ya kukodishia magari ambapo waliiba gari kabla ya kuingia shuleni hapo - Wanafunzi waliouliwa walikuwa wa kiume wengi wao wenye umri kati ya miaka 15 na 16 huku watu wengine 10 wengi wao watoto walijeruhiwa vibaya - Polisi iliwatambulisha washambuliaji hao kuwa ni Guilherme Taucci Monteiro(17) na Luiz Henrique de Castro(25) na kusema kuwa Guilherme ndiye alikuwa kiongozi na mpangaji mkuu - Tukio la mwisho la kufyatuliwa risasi shuleni nchini humo lilikuwa mwaka 2011, ambapo watoto 12 waliuawa mjini Rio de Janeiro #bravotv_tz
#Habari :Rais Dkt.John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Urusi ulioongozwa na mjumbe maalum wa rais wa Urusi katika masuala ya Afrika ambaye pia na naibu waziri wa mambo ya nje Mhe. Mikhail Bogdanov Ikulu jijijini Dar es Salaam. #bravotv_tz
Baba mmoja Mchina aitwae Xu amemfundisha Mbwa wake kumsimamia Mtoto wake wakati akifanya homework ili kuhakikisha Mtoto wake huyo hatumii simu, ni baada ya Baba kuona Mtoto anapenda sana kutumia simu wakati wa masomo nyumbani, ungekua na Mbwa mwenye akili hizi kibongobongo ungependa akuchungie nani? 😄#bravotv_tz (📹‬Pear Video)
Mwaka 1927 charles Lindbergh alikuwa rubani wa kwanza, kurusha ndege kutoka bara moja hadi jingine. In 1927 Charles Lindbergh was the first pilot to fly a solo transatlantic flight. #TBT #AirTanzania #TheWingsOfKilimanjaro #bravotv_tz
Kampuni ya Boeing imetangaza kusitisha matumizi ya ndege zote 371 aina ya Boeing 737MAX8, baada ya ushahidi mpya kuonesha kuwa, visababishi vya kuanguka kwa ndege ya #Ethiopia , vinashabihiana kwa karibu na vile vya ndege ya Lion Air ya nchini #Indonesia . #bravotv_tz
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ashiriki mazishi ya marehemu kaka yake, Mzee Said Majaliwa aliyefariki Machi 12, 2019 na kuzikwa Machi 13.2019 katika kijiji cha Nandagala wilayani #Ruangwa . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) #bravotv_tz
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. @samia_suluhu_hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Africa Now Summit 2019 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort mjini Kampala, #Uganda . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) #bravotv_tz
MKAPA:NCHI MASIKINI HAZIWEZI KUPATA MAENDELEO PASIPO KUWEKEZA ELIMU. Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, amesema nchini masikini haziwezi kupata maendeleo pasipo kuwekeza katika elimu na jukumu hilo linapaswa kutekelezwa na serikali. Mkapa alisema hayo jana, mjini #Morogoro wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya kutimiza miaka 25 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan, mkoani humo. Alisema elimu ndio kila kitu katika taifa lolote na kwamba, ili kuweza kupata maendeleo, lazima kuwa na taifa linalosimamia utoaji wa elimu bora. #bravotv_tz
Mwanafunzi mwingine aokolewa na kupelekwa hospital kupitia umati wa watu na timu ya dharura. kufuatia jengo la shule lililoanguka jijini Lagos, Nigeria. Watu angalau 8 Wamefariki na 37 waokolewa mpaka sasa . #bravotv_tz
RUBANI WA NDEGE YA ETHIOPIA AIRLINE AZIKWA KENYA: Rubani wa ndege ya Ethiopia Airlines iliyoanguka Jumapili na kuua watu 157, Yared Mulugeta Gatechew alikuwa na asili ya Kenya na Ethiopia. Gatechew mwenye umri wa miaka 29 , alizikwa jana na mamia ya waombolezaji katika ibada ya mazishi ya kiislam yakijulikana kama sala ya marehemu asiyekuwepo. Ibada hiyo ilifanyikakatika msikiti maarufu wa Baluch katika mji wa mwambao wa Mombasa nchini Kenya Jumanne jioni. Kwa mujibu wa BBC ndugu wa karibu wa rubani huyo wa ngazi ya juu wanaishi Mombasa, ambako kunatambuliwa kama nyumbani kwa familia yake. #bravotv_tz
PICHA:Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mh.Angellah Kairuki akizungumza na balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke pamoja na wenyeji alioambatana nao wakati wa kikao cha mazungumzo na Waziri Kairuki kuhusu masuala ya fursa za uwekezaji nchini. #england #bravotv_tz
MH. KIKWETE ATEMBELEA UDSM Nimetembelea Maktaba yetu mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya mkutano wangu na Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu. Nimefarijika sana. Ni ya viwango vya kimataifa. "Nimetamani na kukumbukia enzi zangu nikiwa Mwana UDSM na Rais wa DUSO Kampasi ya Mlimani" Ameyasema Hayo JK #bravotv_tz
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (FAA) itasitisha matumizi ya ndege ya Boeing 737 MAX 8 na MAX 9. Nchi mbalinbali zimesitisha matumizi ya ndege hizo, baada ya ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoua watu wote 157 #bravotv_tz
MWANAFUNZI AFARIKI WAKATI AKIOGELEA MTONI - Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tukuyu, Samwel James Chacha (25) amekufa maji akiwa anaogelea kwenye Mto Kiwira uliopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya - Tukio hilo lilitokea Machi 7 na mwili wa marehemu ulipatikana Machi 11 mwaka huu katika Kijiji cha Mboyo, Kata ya Lupepo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwenye mto kiwira - Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya imeeleza chanzo cha tukio ni uzembe wa marehemu kutaka kuogelea kwenye mto huo bila kuchukua tahadhari #bravotv_tz
UCHAGUZI NCHINI ALGERIA WAAHIRISHWA - Uchaguzi wa urais nchini Algeria uliotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi ujao umeahirishwa baada ya Rais Abdelazi Bouteflika aliyetarajia kuwania wadhfa huo kujiondoa - Uamuzi wa kuahirisha uchaguzi huo umetolewa na Rais Bouteflika jana na kusababisha maelfu ya wananchi kuandamana wakidai mabadiliko ya haraka katika nchi hiyo - Abdilaziz Bouteflika (81) ameonekana kukubali shinikizo la waandamanaji ambao wamekuwa wakipinga hatua yake ya kujitosa kwenye kinyanganyiro tena licha ya umri wake na hali yake kiafya #bravotv_tz
WATUMISHI MBARONI KWA WIZI WA DAWA - Watumishi watatu wa idara ya afya Wilayani Chato mkoani Geita wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za wizi wa dawa za aina mbalimbali zinazodaiwa kuwa mali ya Serikali - Kamanda wa Polisi, Mponjoli Mwabulambo amesema kati ya watumishi waliokamatwa, wapo waganga wafawidhi wawili pamoja na mtunza stoo - Dawa zilizokamatwa ni dawa za Malaria aina ya Alu pakiti 1080, mipira ya kuvaa mkononi boksi 10 zinazokaa 50 kwenye kila pakiti - Pia wamekamatwa na vipimo vya Malaria boksi 36, dawa za uzazi wa mpango 41, Alu za watoto pakiti 2,292 pamoja na vipimo vya wingi wa damu - Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kukosa dawa vituoni lakini waganga wafawidhi wamekuwa wakidai dawa zipo na ndipo kamati ya ulinzi iliamua kufanya uchunguzi na kubaini wizi huo #bravotv_tz
Balozi wa China nchini Wang Ke amewasilisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi barua ya pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Wang Yi, kufuatia Profesa Kabudi kuteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hao wameahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya Tanzania na China. #bravotv_tz
NIGERIA: JENGO LENYE SHULE LAANGUKA, WENGI WAHOFIWA KUFA - Jengo la ghorofa tatu lililokuwa na shule ya msingi limeanguka leo majira ya saa nne asubuhi huko Itafaji jijini Lagos ikiwa ni muda ambao vipindi vimeanza shuleni - Shule hiyo inadaiwa ilikuwa katika ghorofa ya juu na watu wengi wakiwemo watoto wanahofiwa kufa kwa kufukiwa na vifusi - Hadi sasa taarifa zinasema ni watu kadhaa wakiwemo watoto wameokolewa kutoka kwenye vifusi na uaokoaji unaendelea huku kukiwa hakuna taarifa za vifo - Sababu za jengo hilo lililokuwa na makazi ya watu katika ghorofa nyingine mbili kuanguka bado hazijafahamika - Aidha, nchini Nigeria mwaka 2016 zaidi ya watu 100 walifariki baada ya paa la Kanisa huko Uyo, Kisini mwa nchi kuanguka na pia watu 30 walifariki Lagos baada ya jengo lililokuwa linajegwa kuanguka mwaka huo huo #bravotv_tz
WATAALAMU WA ATOMIKI WAKUTANA, TANZANIA NI MMOJA WA WANUFAIKA - Wataalamu wa Nguvu za Atomiki kutoka nchi 46 za Afrika wamekutana Arusha kujadili utekelezaji miradi ya matumizi salama ya Sayansi na Teknolojia ya nyuklia katika nchi zao - Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema wamekutana kuweka mikakati ya matumizi sahihi ya Atomiki - Nchi za Afrika zimepata manufaa makubwa katika matumizi ya Atomiki hususani Tanzania ambayo imepata Tsh bilioni 9 zinazotekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ununuzi wa vifaa tiba vya kuchunguza Saratani katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam na Bugando jijini Mwanza - Aidha, wanaendelea kupata mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kudhibiti mionzi isilete madhara #bravotv_tz
Doreta Norris wa Marekani ambae alikuwa akisumbuliwa kansa ya Matiti akicheza wimbo wa ‘Gangnam Style’ na Madaktari wake pamoja na Wauguzi hospitalini kabla ya kuingizwa katika chumba cha operesheni, inaelezwa kwa sasa Doreta hana tena maradhi hayo.(📹 Piedmont Healthcare) #bravotv_tz
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu asisitiza utawala Bora akiwa mjini Kampala nchini Uganda. #bravotv_tz
#UefaChampionLeague Cristiano Ronaldo aivusha Juventus hatua inayofuata baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya A.Madrid. #bravotv_tz
MAREKANI KUWAONDOA WANADIPLOMASIA WAKE VENEZUELA - Marekani kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje imesema itawaondoa wafanyakazi wake wote wa ubalozini waliobakia nchini Venezuela kwasababu hali imezidi kuwa mbaya nchini humo - Mike Pompeo amesema uwepo wa wafanyakazi hao wa ubalozi nchini Venezuela unazuia hatua ambazo utawala wa Marekani ungeweza kuchukua juu ya Venezuela - Rais wa Venezuela Nicolas Maduro alishavunja uhusiano wa kibalozi baina ya nchi yake na Marekani mnamo mwezi Januari baada ya Marekani kutangaza kumuunga mkono kiongozi wa upinzani, Juan Guaido #bravotv_tz
Shule moja ya sekondari huko kusini mwa China imeingia matatani baada ya kuanzisha programu ya kuwafuatilia wanafunzi kwa kuwavika kifaa maalumu ambacho pamoja na mambo mengine kitakuwa kinaripoti ni mara ngapi mwanafunzi amenyoosha mkono darasani. Kifaa mfano wa bangili kinahusishwa na kufuatilia mwenendo, mapigo ya moyo, shughuli anazofanya mwanafunzi na hata mahudhurio yake huku mfumo huo ukikosolewa vikali kwa kuingilia faragha za mwanafunzi kwa kwamba hauna tofauti na ule wa mfungwa. #bravotv_tz
"Yeyote anayetaka kuvunja amanai ya nchini hawezi kuachwa hivi hivi, hawezi kujua nguvu yetu ni kubwa sana na hawezi kuendelea kuishi kwa amani, nakuhakikishia wewe ambaye ni msumbufu wa nchi yangu" Rais wa Uganda - Yoweri Museveni. #bravotv_tz
"Mimi nimekuwa nikishangaa sana kila mwaka kumekuwapo na sherehe za upandaji wa miti milioni moja lakini sijawahi kuona matokeo yake, nazunguka sana wakati nikitekeleza majukumu yangu, sijawahi kuonyeshwa kijiji au pori" Waziri wa Maliasili - Hamisi Kigwangalla. #bravotv_tz
"Mkosefu wa hovyo ni yule anayekosa halafu hataki kurekebishwa" Kheri James Nini maoni yako katika kauli hii? #bravotv_tz
Baada ya kurejea tena katika kikosi cha Real Madrid, Kocha Zinedine Zidane ameanza kazi rasmi leo akikabiliwa na kibarua kigumu cha kurejesha makali ya Madrid ambayo tayari imeondolewa katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa kufungwa bao 4-1 dhidi ya Ajax. Je, unadhani kwa sasa ataweza kurejesha makali ya klabu hiyo kama zamani? #bravotv_tz
Madaktari Bingwa wa MOI na Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo kupitia kwenye tundu la pua (Endoscopic Trans nasal transsphenoidal pituitary surgery). Awali upasuaji huo ulikuwa haufanyiki hapa nchini. #bravotv_tz
KUKOSEKANA KWA UMEME VENEZUELA: WATU 17 WAPOTEZA MAISHA - Kwa mujibu wa kiongozi wa upinzani, Juan Guaido mpaka sasa ikiwa inakaribia siku ya 5, baadhi ya maeneo muhimu hayana umeme ikiwemo Hospitali na watu takribani 17 wamepoteza maisha kwa kushindwa kufanyiwa upasuaji - Rais Nicolas Maduro ameishutumu Marekani kuwa ndio walioshambulia miundombinu ya umeme nchini humo, japo amekiri kuwa bado hawajathibitisha hilo - Shughuli mbalimbali ikiwemo shule na ofisi za Serikali nchini Venezuela, zimesitishwa kwa saa 48 kuanzia jana(Machi 11) kutokana na kukosekana kwa umeme nchi nzima tangu Alhamisi mchana(Machi 7) - Imeelezwa kuwa hitilafu kubwa imetokea katika mitambo mikuu ya kuzalisha umeme katika mji mkuu wa Venezuela Caracas hivyo kusababisha kukosekana kwa umeme katika eneo kubwa la nchi #bravotv_tz
ZITTO ATAKIWA KUELEZA SABABU ZA KUTOFIKA MAHAKAMANI - Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wadhamini wake, kufika Mahakamani kujieleza kwanini hawakufika kwenye kesi jana - Amri hiyo ilitolewa jana na Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa utetezi, Steven Mwakibolwa kudai kuwa amepata taarifa kutoka kwa shemeji wa mshtakiwa kwamba Zitto ni mgonjwa lakini hafahamu mahali alipo - Katika kesi ya msingi, inadaiwa kuwa Oktoba 28, 2018 akiwa Makao Makuu ya ofisi za Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki #bravotv_tz
MKUU WA MKOA MBEYA: UKIIBIWA MUME/MKE NITUMIE UJUMBE - RC Albert Chalamila amewaambia wakazi wa Mbeya atakaye kuwa wakiibiwa Mume/Mke wamtumie ujumbe kwenye simu na yeye atashughulika na mwizi huyo - Akiwa Matundasi amesema kabla ya kuondoka ataacha namba yake ya simu na kuwataka Wananchi wamtumie ujumbe muda wowote ila usipige - Amewaasa wasimpigie simu kwani hataweza kusikiliza kila simu itakayopigwa #bravotv_tz
AJERUHIWA KWA KITU CHENYE NCHA KALI KWENYE KORODANI - Mwanamume mmoja, mkazi wa Moshi mwenye umri wa miaka 53, amejeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika korodani moja - Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea saa nne usiku Machi 7 katika eneo la Marera, Moshi - Watuhumiwa ni vijana wawili wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lyakrimu; wa kiume (18) na wa kike (14) ambao tayari wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa kuhusika kwenye tukio hilo - Majeruhi amelazwa Hospitali ya Kilema akiendelea na matibabu na chanzo cha tukio bado hakijajulikana #bravotv_tz
ILALA, DAR: ALIYESHTAKIWA KWA SHERIA ZA NJE AACHIWA HURU - Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuachia huru, Isidory Karume (57) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kukutwa akimiliki risasi mbili za bastola - Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya kubainika sheria iliyotumika kumshtaki haipo Tanzania - Alikamatwa Januari Mosi, 2018 akiwa na risasi hizo bila ya kuwa na kibali. #bravotv_tz
Orodha ya Mataifa yaliyositisha safari za Ndege aina ya Boeng 737 Max 8 kupisha uchunguzi - China, UK, Germany, France, Mexico, Brazil, Argentina, Indonesia, Turkey, Ireland, Australia, Ethiopia, South Africa, Malaysia, Singapore, Oman, Morocco na Mongolia #EthiopianAirlinesCrash #bravotv_tz
SHERIA YA HALI YA HATARI NCHINI SUDAN YAPUNGUZWA MUDA - Muda wa kutekelezwa sheria ya hali ya hatari nchini Sudan umepunguzwa kutoka mwaka mmoja na sasa ni miezi sita - Tangazo la Bunge la Sudan la kupunguza muda wa utekelezwaji wa sheria ya hatari kutoka mwaka mmoja hadi miezi sita linatolewa huku wananchi wakiwa kwenye maandamano dhidi ya Serikali - Hivi karibuni shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilitangaza kwamba watu karibu 60 wameuawa hadi sasa tangu kuanza kwa maandamano hayo #bravotv_tz
ARUSHA: WAKAZI WADAIWA KUKUMBWA NA UGONJWA WA KUHARA ULIOSABABISHWA NA MAJI - Baadhi ya wakazi hao wa maeneo tofauti wanadaiwa kuwa na hali mbaya kiafya na wengine kulazwa katika Hospital ya Mount Meru kutokana na kunywa maji yanayodaiwa kuchanganyikana na majitaka wakati wa ujenzi wa mfumo wa majisafi na majitaka katikati ya Jiji la Arusha - Hali hiyo imeripotiwa katika maeneo ya Sinoni, Daraja mbili na katikati ya Jiji la Arusha huku mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira AUWSA ikikanusha hali hiyo kwa madai kuwa maji yanayotumika jijini hapa ni salama na hayana madhara - Baadhi ya wakazi wamedai kuwa maji wanayokunywa yanayotoka kwenye mfumo wa mabomba ya AUWSA yamechanganyikana na majitaka na takribani wiki sasa wanalalamikia maji hayo na hakuna msaada wowote kutoka mamlaka husika. #bravotv_tz
UINGEREZA: BUNGE LAUKATAA MPANGO WA BREXIT - Bunge la Uingereza laukata mpango wa nchi hiyo kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya uliowasilishwa na Waziri Mkuu, Theresa May - Kura 391 zaukataa mpango huo huku Wabunge 242 wauukiunga mkono mpango huo - Theresa May anashindwa kulishawishi Bunge zikiwa zimesalia siku 17 kabla ya kuanza kuutekeleza mpango huo - Kura hiyo dhidi ya Theresa May inaweza kuibua hoja ya kutokuwa na imani naye na kama atashindwa basi nchi hiyo itarudi kwenye tena uchaguzi. #bravotv_tz
Polisi wa Uingereza wameanza kufanya uchunguzi baada ya baadhi ya Polisi wake kuonekana katika video wakimpiga Mtu mweusi.#bravotv_tz (📹rt)
Mkurugenzi wa Makampuni ya Kilua, Mohammed Kilua ni miongoni mwa Watanzania wanaozunguka nje ya Nchi kufanya mikutano ya kutafuta Wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, hapa ni Dar es salaam wakati akipokea zawadi na cheti kutoka kwa Wachina aliowatoa China kuja kujionea fursa za kuwekeza Tanzania. #bravotv_tz
Mwanafunzi huyu aitwae Tanner Wilson wa Caddo Hills High School nchini Marekani amepokea sifa baada kutunza fedha zake kwa miaka miwili ili aweze kumnunulia rafiki yake Brandon Qualls wheelchair ya kielektroniki, awali Qualls alikuwa akitumia wheelchair ya kujisukuma kwa mikono na Mwalimu wa Wilson amesema Mwanafunzi huyo anapenda sana kujitoa kwa ajili ya Watu wengine.(📹 CNN) #bravotv_tz
Kiungo wa Arsenal Ozil amemzawadia jezi 2 za Arsenal zilizo sainiwa pamoja na pea za viatu Mtoto Lawrence Masira (9) wa nchini Kenya baada ya picha yake akiwa anachunga Ng’ombe huku akiwa amevalia jezi bandia yenye namba ya Ozil kusambaa mtandaoni na kumfikia Kiungo huyo.#bravotv_tz
"Wewe mkuu wa wilaya au mkurugenzi una gari zuri, nyumba, mshahara, posho nyingi, maji, umeme kwa nini ugombane na mwenzako? Ni ujinga na haufai kuitwa kiongozi," - Antony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa #Simiyu . #bravotv_tz TOA MAONI YAKO HAPA
“Tunachotaka kujua ni kama Mtoto wetu yupo sawa kiakili na kimwili” Mama wa Joycelyn Savage ( mmoja wa Wapenzi wa R. Kelly) akizungumza kuomba kukutana na Mwanae huyo baada ya kupita miaka miwili bila kuonana, hatua hii ni inakuja baada ya Mwanae huyo kumtuhumu yeye pamoja na Mume wake kumtishia Mwimbaji R. Kelly ili wajipatie fedha.#bravotv_tz (📹 CBS)
UUZAJI WA SILAHA DUNIANI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 8 - Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa masuala ya amani duniani, SIPRI imesema uuzaji wa silaha za kivita duniani umeongezeka kwa kiasi cha asilimia 8 katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2018 ikilinganishwa na 2009 hadi 2013 - Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo, Marekani inaongoza kwa kuuza silaha duniani, ambapo imesafirisha zaidi ya theluthi ya silaha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita - Marekani imesafirisha asilimia 36 ya silaha zote zilizouzwa kati ya mwaka 2014 na 2018, hiyo ikiwa ni asilimia 6 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2009 hadi 2013 - Taasisi hiyo yenye makao yake mjini Stockholm, Sweden imesema Marekani imeuza silaha kwa nchi zipatazo 98 duniani, huku nusu yake zikiwa zimeuzwa katika eneo la Mashariki ya Kati #bravotv_tz
FAHAMU MAMBO YA MSINGI KATIKA KILIMO CHA MIHOGO - Zao la muhogo ni muhimu sana na zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Unaweza kulima kwa kuchanganya na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe - Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka - Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga na ni zao maarufu sana kwa uvumilivu kwenye hali ya ukame - Kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimethibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji. - Mbegu ya Naliendele huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe na mbegu ya Kiroba huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe - Shamba liandaliwe kabla ya msimu kuanza na uandaaji wa shamba bora hufuata hatua ikiwemo Kufyeka shamba, Kungo’a na kuchoma visiki halafu Kulima na kutengeneza matuta #bravotv_tz
TANZANIA YAONGOZA KWA KUWA NA SIMBA WENGI BARANI AFRIKA - African Wildlife Foundation imesema Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na Simba wengi na kwa upande wa Tembo inashika nafasi ya tatu barani Afrika - Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation, Kaddu Sebunya wakati akizungumzia umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori na uhifadhi wa mazingira kwa nchi za Bara la Afrika - Nchi inayoongoza kwa kuwa na Tembo wengi ni Botswana ikifuatiwa na Zimbabwe - Hata hivyo, Sebunya amesema kwa sasa kuna changamoto ya wanyamapori wengi hasa Simba na Tembo kupungua na sababu yake ni uwepo wa majangiri na uwindaji haramu #bravotv_tz
WANAWAKE WALIOANDAMANA SUDAN WAHUKUMIWA KWENDA JELA - Mahakama ya Khartoum imemhukumu kifungo cha wiki moja jela Naibu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani cha Umma, Mariam Sadiq al-Mahdi pamoja na wanawake wengine wa upinzani na kuwatoza faini ya pauni elfu 2 za Sudan (dola 42) kwa kushiriki maandamano ‘haramu’ - Mariam Sadiq al-Mahdi ni binti wa mkuu wa chama cha Umma, Sadiq al Mahdi ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa mwisho aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini Sudan - Siku kadhaa zilizopita, Rais wa Sudan alivunja Serikali na kutangaza hali ya hatari nchi nzima na kisha akawafuta kazi Magavana wa mikoa yote ya nchi hiyo na nyadhifa hizo kukabidhiwa wanajeshi - Sudan kumekuwa na maandamano ya wananchi tangu Desemba 19, 2018 wanaolalamikia hali ngumu ya kiuchumi na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu hususani bei ya Mkate na Petroli #bravotv_tz
Habari:Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeshindwa kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe baada,kushindwa kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa.#bravotv_tz
Viongozi wa dini na wananchi mbalimbali wameitaka Serikali kudhibiti wimbi la manabii wanaodaiwa kutoa mafundisho potofu ambayo ni hatari, kwa upande wake Askofu wa KKKT Fredrick Shoo, ameiomba Serikali kuweka sheria kwa wachungaji wote kuwa na elimu ya Thiolojia. #bravotv_tz
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewaagiza makamada wa polisi nchini washirikiane na wakuu wa mikoa kuchunguza na kuwakamata wapinzani wanaomtukana Rais na Serikali kupitia vikao vya ndani vya siasa huku akiwataka wapinzani kuwa wasikivu na kufuata sheria. #bravotv_tz
"Chadema walimfananisha Lowassa na tembo wa siasa, lakini kwetu sisi Lowassa ni hazina" Shaka Hamdu Shaka. #bravotv_tz
Mbunge wa Tarime vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche amekabidhi mabati 100 kwa ajili ya kukamilisha vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Sirari. #bravotv_tz
#UNAAMBIWA Forbes imemtaja Mwanamitindo Kylie Jenner (21) kama Bilionea mdogo zaidi Duniani, utajiri wa Kylie unatokana na biashara yake ya vipodozi (Kylie Cosmetics) ambayo kwa mwaka 2018 inatajwa kumuingizia zaidi ya Tsh. Bilioni 846 , Kylie amefikia Ubilionea akiwa na umri mdogo zaidi akimzidi Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg aliyefikia Ubilionea akiwa na miaka 23.#MillardAyoUPDATES (📹 CGTN) #bravotv_tz
Makamu wa Rais kumuwakilisha Rais Dkt Magufuli mkutano wa Africa Now Summit 2019 nchini Uganda Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @samia_suluhu_hassan anaondoka nchini leo kuelekea Kampala, #Uganda kushiriki kwenye Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika tarehe12 na 13 Machi.Mhe. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huu. Mkutano utakuwa na mada mbalimbali ikiwemo ya Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika, mada hii itatolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. #africanowsummit19 #bravotv_tz
CHINA, ETHIOPIA ZASITISHA KUTUMIA BOEING 737 MAX 8 - China imeyaamuru mashirika ya ndege ya ndani ya nchi kusimamisha matumizi ya ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 kufuatia ajali ya ndege iliyotokea Ethiopia na ajali nyingine kama hiyo iliyotokea nchini Indonesia - Imesema kuwa operesheni ya kutumia ndege hizo itaanza tu baada ya kuthibitisha kuwa ndege hizi zinafaa kwa matumizi na ni salama - Shirika la ndege la Ethiopia nalo limetangaza kusitisha safari za ndege zake zote aina ya Boeing 737 Max 8 kuanzia Machi 10 mwaka huu - Wameamua kuchukua hatua hiyo kama tahadhari ya ziada licha ya kuwa bado chanzo cha ajali iliyotokea jana bado hakijafahamika mpaka sasa - Ajali ya Ethiopia jana ilisababisha vifo vya abiria 157 huku 8 kati yao wakiwa raia wa China #bravotv_tz
Kampuni ya kuunda ndege kutoka Marekani Boeing imeahirisha uzinduzi wa ndege yake mpya na ya kisasa zaidi ya kubeba abiria ya Boeing 777X Jetliner ilikukabiliana na ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines #et302 iliyoanguka ikielekea Nairobi kutoka uwanja wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa. Ndege hii mpya inauwezo wa kubeba takriban abiria 425.📸: Getty #ethiopian #ethiopianairlines #bravotv_tz
Mfanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Marekani, Mooney (31) akipewa escort hospitalini kama ishara ya kumpa heshima wakati akipelekwa kutoa baadhi ya viungo vyake vya mwili ili vikasaidie Watu wengine baada ya uvimbe aliokuwa nao kwenye ubongo wake kushindikana kupona na hivyo kutambua kwamba alibakiza muda mfupi sana wa kuishi duniani, Marafiki, Madaktari, Familia pamoja na Wafanyakazi wenzake walikuwepo wakati Mooney akivuta pumzi yake ya mwisho, ameacha Mke na Watoto wanne.(📹 CBS) #bravotv_tz
Operesheni ya utafutaji ikiendelea kwenye eneo ambalo Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia aina ya Boeing 737 MAX 8 ilianguka jana na kusababisha vifo vya Watu wote 157 waliokuwemo ndani.#bravotv_tz ( AFP TV)
Je, unadhani wakati umefika kwa wahandisi wasiofuatilia miradi mbalimbali kwa ukaribu inayoligharimu taifa fedha nyingi wabadilike ili miradi husika itekelezwe kwa ufanisi zaidi? #bravotv_tz
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumapili Machi 10, 2019. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa. @ikulu_mawasiliano @gersonmsigwa #bravotv_tz
IRAN: WAPENZI WAKAMATWA BAADA YA KUCHUMBIANA HADHARANI - Wapenzi hao walikamatwa kwa kosa la kukiuka maadili ya kidini ambapo nchini humo kuonesha hadharani mapenzi kumepigwa marufuku - Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha wapenzi hao wakiwa wamesimama katika mzunguko uliotengenezwa kwa maua wakiwa pia wamezungukwa na watu - Inaonekana Mwanamke akikubali ombi la Mwanaume na kumkumbatia huku watu waliowazunguka wakiwashangilia kwa furaha - Naibu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Markazi, Mahmoud Khalaji ameliambia shirika la habari la Fars nchini humo kuwa Wachumba hao wametiwa mbaroni kwa 'maslahi' ya umma - Amesema wamekamatwa kwa ukiukaji mkubwa wa maadili kwa kufanya kitendo hicho ambacho kimechochewa na utamaduni wa mataifa ya Magharibi #bravotv_tz
TCRA YAFICHUA 'MADUDU' VITUO VYA REDIO KANDA YA ZIWA - Mamlaka Mawasiliano Tanzania yatoa miezi minne kwa vituo hivyo kurekebisha mapungufu mbalimbali yaliyobainika walipofanya ukaguzi kwenye vituo takribani 36 - Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Injinia Francis Mihayo amesema wanatakiwa kufanya marekebisho vinginevyo wataamuriwa kusitisha huduma mpaka watakapojirekebisha - Ataja mapungufu yaliyopo kuwa pamoja na wafanyakazi kutokuwa na mikataba ya ajira, Watangazaji kuwa na elimu ya darasa la saba, Kidato cha Pili au Kidato cha Nne pamoja na kazi kutolewa kiukoo - Mengine ni vituo kukosa vyoo au kuwa na vyoo vichafu, studio kutokuwa sound proof na ukosekanaji wa ubunifu katika kutafuta habari na kupelekea ratiba kubadilishwa kiholela bila kuitaarifu TCRA - Kuhusu mapungufu ya sifa za waajiriwa, amesema Serikali ilitoa muda mpaka Desemba 2019 kila kituo lazima kiwe na wanahabari wenye kima cha chini cha elimu ya Stashahada na si vinginevyo #bravotv_tz
next page →